Shirika la habari la "Hawza" - Kwa mujibu wa ripoti ya IQNA iliyotolewa na Ofisi ya Mahusiano ya Umma na Habari ya Shirika la Utamaduni na Mahusiano ya Kiislamu (ICRO), katika katika moja ya vikao hivyo, qari huyo alijumuika na Maulamaa wa Kishia, Waislamu wa Kenya, maafisa wa ubalozi wa Iran jijini Nairobi na na familia za Wairani nchini Kenya. Akizungumza katika hafla hiyo Dkt. Pourmarjan Ghorbanali, mwabata wa utamaduni wa Iran nchini Kenya alisema: Qur’ani daima ina umuhimu kwa Waislamu, lakini katika mwezi mtukufu wa Ramadhani ambao ni mwezi wa karamu ya Mwenyezi Mungu; Qur’ani ina umuhimu wa kimsingi na usomaji wa Qur’ani, kusikiliza Qurani na kufuata maelekezo ya Qur’ani yanapaswa kuwa kipaumbele chetu cha kwanza.”
Aidha alisema: Qur’ani katika familia ya Muislamu na jamii ya Kiislamu haipaswi kuwa imeachwa, kwa kuwa ni kitabu cha mbinguni na ni moja ya amana mbili za Mtume Muhammad (SAW) kwa ajili yetu baada ya yeye mwenyewe ambacho alituachi ambazo ni Qur’ani na Ahlul-Bayt (AS).
Aliongeza kuwa: “Natumaini katika mwezi mtukufu wa Ramadhani tutafaidika vya kutosha na nuru ya Qur’ani, kwa kuwa Imam Ali (.S) alisema kuwa Qur’ani ni chemchemi ya moyo na mwezi wa Ramadhani pia ni chemchemi ya Qur’ani.
Katika mwendelezo wa hafla hii, Ustadh Ahmad Aboulghasemi, mmoja wa wasomaji wa kimataifa kutoka Iran ambaye ameenda Kenya kwa ajili ya kuwa jaji wa mashindano ya Qur’ani katika mji wa Mombasa na kusoma katika misikiti na vituo vya redio na televisheni, alisoma aya za Qurani Tukufu.
Chanzo: IQNA
Maoni yako